asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, December 14, 2016

Aliyetobolewa macho uso kwa uso na Scorpion mahakamani

Tokeo la picha la scorpion mtoboa macho
Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Ilala wakati shauri hilo lilipoletwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Picha inayohusiana
Wakati mshitakiwa akipandishwa kizimbani alidai ana wakili wake hivyo mahakama ilisubiri kwa muda wakili wa mshitakiwa Juma Nassoro na baada ya kufika mahakamani ndio kesi ilianza kusikilizwa.
Kesi hiyo ina mashahidi sita na mpaka sasa ameshasikilizwa mmoja ambaye ni shahidi namba moja Said Mrisho ‘aliyetobolewa macho’ ambaye leo December 14 2016 ametoa ushahidi wake mahakamani hapo akielezea tukio alilofanyiwa.
Baada ya kusikiliza kesi, mahakama hiyo imeahirisha shauri hilo hadi December 28 mwaka huu ambapo itaendelea na shahidi wa pili.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt