asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, May 21, 2017

HATIMAYE UBINGWA WA YANGA WAINGIA DOSARI,...!! SIMBA WASIMAMA KIDETE..TAZAMA HAPA WALICHOAMUA

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba imewasilisha malalamiko ya barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa pointi 3, hatimaye uthibitisho wapatikana.


Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha vielelezo hivyo, imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli Simba kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.

Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja itatangazwa kuwa bingwa.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba aliyefungiwa, Haji Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa, soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"

Halafu akaendelea;........"Hivi unadhani FIFA wana figisu guys?kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu,no way out!!ukizingatia repoti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti!SHUBAMIT"


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt