asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, May 7, 2017

SI RUVU SHOOTING, SI YANGA, SI SIMBA,...!! VUTA NIKUVUTE YA KIATU CHA DHAHABU CHA MFUNGAJI BORA VPL SASA YAFIKA PATAMU...HII HAPA ORODHA YA MIAMBA WANAOWANIA KIATU HICHO...

Image result for GOLDEN SHOESu
Mchezaji bora wa mwezi April 2017 Abdulrahman Mussa amemtoa Simon Msuva kwenye nafasi kwanza ya orodha ya wafungaji wa msimu huu kwenye ligi kuu Tanzania bara.
Mchezaji huyo alifunga goli lake la 13 kwenye ligi wakati timu yake ya Ruvu Shooting ipolazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
Vyanzo vingine vinasema Abdulrahman Mussa hakufunga goli hilo bali goli lilifungwa na Fuluzuru Maganga baada ya kutokea piga nikupige kwenye goli la Kagera Sugar.
Shaffihdauda.co.tz bado inaendelea kufutilia kwa karibu zaidi ili kujua ni nani hasa alifunga goli hilo ili kujiridhisha bila shaka juu ya utata uliopo sasa.
Orodha ya wachezaji wanaochuana kwenye kinyang’anyiro cha ufungaji bora ligi kuu Tanzania bara 2016/17
Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting) 13
Simon Msuva (Yanga) 12
Shiza Kichuya (Simba) 11
Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar) 11
Obrey Chirwa (Yanga) 10
Amis Tambwe (Yanga) 10
John Bocco (Azam) 10


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt