asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, January 31, 2017

Waziri Mkuu apokea ugomvi wa DC ,Mkuu wa wilaya


Dodoma. Mgogoro baina ya Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia na mkuu wa wilaya hiyo, Saimon Odunga umechukua sura mpya, safari hii ukiibuka katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dodoma (RCC) ambayo imeamua ufikishwe kwa Waziri Mkuu.

Kikao hicho ambacho kilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kilifanyika  katika ukumbi wa Chuo cha Mipango.

Baada ya Odunga kupewa nafasi ya kuchangia ajenda mara baada ya Majaliwa kuondoka, aliomba ushirikiano kutoka kwa wabunge ilikutekeleza shughuli za maendeleo.

“Ninaomba waheshimiwa wabunge watusaidie kulisemea hili kwa sababu hali ni mbaya katika sekta nyingi,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho, Nkamia, ambaye aliwahi  kuwa naibu waziri, alianza kwa kumuomba Rugimbana kusaidia katika sekta ya ardhi akisema ina matatizo mengi na kutoa mfano wa Wilaya ya Chemba.

Alisema katika wilaya hiyo kuna tapeli wa ardhi ambaye amesaidiwa na viongozi kupata ardhi yenye ukubwa wa ekari 500 kinyume na sheria.

Alihoji sababu za mkuu huyo wa wilaya kutaka wabunge washiriki katika kusukuma hoja mbalimbali za maendeleo, wakati anadharau wabunge, mwenyekiti wa halmashauri na viongozi wengine wa chama wilayani humo.

“Huyu ni mkuu wa wilaya ambaye anaongoza kwa rekodi ya kuwakamata watu kwa kutumia madaraka yake. Nimesikia jana (juzi) kuwa na mimi nawindwa ili nikamatwe. Niko tayari kukamatwa,” alisema Nkamia, ambaye anaongoza Jimbo la Chemba kwa kipindi cha pili mfululizo.

“Nakuomba mkuu wa mkoa umuite huyu dogo (DC) umkanye kuhusu hii tabia yake ya kudhalilisha watu. Kwa kuwa bwana mkubwa (DC) hapo ameanzisha vita na sisi tunaomsaidia kazi. Sisi tuna busara zetu, hatuwezi kuingia vitani,” alisema.

Nkamia alimuomba Rugimbana kuwaita wote wawili-Odunga na yeye-wakae pamoja na kutafutia suluhu ya jambo hilo ambalo alisema linaweza kukwamisha maendeleo ya jimbo hilo.

Alimuonya mkuu huyo wa wilaya kuhusu tabia ya kuwatia mbaroni wananchi wanaouliza maswali wakati ni haki yao kufanya hivyo.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt