Maishani, watu wengi hutaka kuishi
katika nyumba nzuri na za kifahari. Wengi huwa hawafanikiwi. Lakini
nchini Mexico, ambapo ulanguzi wa mihadarati umekithiri, wakuu wa
magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya huishi maisha ya kifahari, na
huendeleza hizi hata wanapokuwa wafu.
Nchini humo, utapata makaburi ambayo yangegeuzwa kuwa nyumba, matajiri wengi wangejivunia kuishi.Ni makaburi makubwa yaliyojengwa na kuwekwa huduma za kisasa na vitu vingi vya anasa.
Kuna baadhi ya makaburi yenye viyoyozi vya kudhibiti viwnago vya joto na kuingiza hewa safi, kuna vioo visivyopenya risasi na baadhi yana hata vyumba ambavyo wageni wanaofika kutoa heshima kwa wafu, wanaweza kuketi na kupata kila kitu kinachopatikana katika nyumba za kifahari.
Baadhi yanakadiriwa kugharimu hadi £230,000 (Sh633 milioni za Tanzania; Sh29 milioni za Kenya)
Hali hii ni tofauti kabisa kwa maelfu ya watu wanaouawa katika makabiliano ya magenge ya ulanguzi wa dawa hizo za kulevya ambao sana huzikwa katika makaburi ya pamoja au miili yao kutungikwa na kuachwa ikiwa imening'inia kwenye madaraja.
Lakini walanguzi wakuu, ambao wamejipatia pesa nyingi, wanaweza kupamba makaburi yao kutokana na pesa walizolimbikiza kutokana na biashara hiyo.
Katika eneo moja la makaburi, Jardines del Humaya, katika mji mkuu wa jimbo la Culiacan, ndipo unapopata baadhi ya makaburi ya kupendeza zaidi.
"Pia ni onesho kwa wale ambao wanaendelea kuishi kwamba mtu huyu alikuwa mtu mashuhuri."
"Ulanguzi wa mihadarati unakolea katika jamii, kupitia utamaduni, na sasa tuna tatizo la kutazama umeanzisha wapi na umefikia mwisho wapi," alisema Ayala.
Lina pia kuba lenye taa ambazo huwaka. Ndani kuna visu vinne vilivyofungiwa kwenye kijisanduku kilichoundwa kwa vioo.
Lakini kinachokosekana katika makaburi mengi ni utambulisho wa aliyezikwa ndani.
"Kuna mchango mkubwa wa dini katika utamaduni wa ulanguzi wa dawa, kwa sababu iwapo kuna mtu anayehitaji sana ulinzi kutoka kwa miungu au Mungu, basi ni mlanguzi wa mihadarati ambaye anaweza kuuawa kwa kupigwa risasi na magenge hasimu au maafisa wa serikali wakati wowote," anasema Andrew Chesnut, mwandishi wa kitabu kwa jina Devoted to Death: Santa Muerte, the Skeleton Saint (Kujitolea kwa Kifo: Santa Muerte, Mtakatifu wa Kiunzi cha Mifupa)
No comments:
Post a Comment