asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, December 5, 2016

HII NDIO SABABU YA MTOTO WA DARASA LA TANO KUJINYONGA

Dodoma. Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kizota mjini hapa, Yasin  Abdallah (13) amekutwa amejinyonga bafuni nyumbani kwao baada ya kuchukizwa kufanya vibaya kwenye masomo yake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimoli alisema tukio hilo lilitokea Desemba 2 eneo la Kizota Relini Manispaa ya Dodoma.

Kimoli alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Hassan Juma (53) aligundua kujinyonga kwa mwanaye saa 6:00 mchana. “Sababu ya kujinyonga ni kuchukizwa na matokeo ya mitihani yake,” alisema.

Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga. Alisema baada ya kutamka maneno hayo, wenzake walimwambia wanakwenda kumweleza mwalimu.

Hata hivyo, baada ya kuwasikia  wenzake aliwaambia kuwa anatania hawezi kufanya hivyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kizota, Juma Malecela alisema mwanafunzi huyo alihamia Oktoba kutoka mkoani Kigoma.


“Katika matokeo ya kumaliza darasa la nne alikuwa wa 129 kati ya 132, inawezekana huko alikuwa anafanya vizuri,” alisema.

 lakini alipofika hapa matokeo yakawa tofauti,” alisema.

Alisema siku ya Ijumaa ilikuwa ni siku ya kufunga shule ambapo wanafunzi waliruhusiwa saa 4.30 asubuhi baada ya kupatiwa ripoti.

“Tukiwa kwenye kikao cha walimu shuleni nilipata simu kutoka kwa ofisa mtendaji kuwa Yasini amejinyonga nyumbani. Lakini inawezekana kuwa wazazi wake walimsema walivyoona ameshindwa kufanya vizuri,”alisema.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt