asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, December 16, 2016

Kafulila ahama NCCR, ahamia Chadema


Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila leo ametangaza kukihama chama hicho na kusema kuwa atajiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA).

Kafulila ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika bunge la kumi kwa kufichua hoja mbalimbali za ufisadi amesema kuwa ameshawasilisha barua ya kujiuzulu kwa uongozi wa chama hicho.

Akieleza sababu iliyomsukuma kujiunga na CHADEMA, Kafulila alinukuliwa akisema kuwa kikubwa ni kuhakikia wanaleta mabadiliko nchini Tanzania. 
"Ili kufanya safari kuwa fupi, kuondoa vikwazo vya huyu yuko chama hiki mwingine kile nimemamua kujiunga na CHADEMA ili kurahisisha uletaji mabadiliko katika nchi yetu sababu nimeona uhitaji huo," alisema Kafulila.

Katika uchaguzi uliopita Kafulila alipoteza jimbo la Kigoma Kusini ambalo lilikwenda wa Hasna Sudi Katunda Mwilima aliyekuwa akigombea kupitia Chama cha Mapinduzi


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt