asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, December 11, 2016

KUNDI LA WATU WASIOJULIKANA LAWA TISHIO ARUMERU

Kundi la watu wasiojulikana  linalosadikiwa  kupiga kambi katika msitu wa mto  Meru uliopo kijiji cha  Olgilayi  wilayani Arumeru limekua tishio kwa maisha ya wanawake  na watoto wanaokwenda kuokota kuni  katika msitu huo kwa  kuwakamata na kuwafanyia vitendo vya  kinyama  vikiwemo vipigo na kutishiwa kubakwa.

Wakizungumza kijijini Olgilayi wanawake waliopatwa na mkasa wa kusulubiwa na watu hao wanasema wamekua wakilazimishwa kufanya vitendo vya ngono na pale wanapokataa hupewa adhabu ya kipigo.

Matukio hayo yamewalazimu baadhi ya wazee na vijana kukutana na kuiomba  serikali kuchukua hatua za haraka kukabiliana na kundi hilo ambalo mwenyekiti Emanuel Lukumai anasema wameshalitolea taarifa lakini bado hakuna hatua zilizochukuliwa.

ITV imemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo kwa njia ya simu  kuthibitisha tukio hilo ambalo limetolewa taarifa kituo cha polisi Usa River na waliojeruhiwa kupatiwa RB za shambulio la mwili lakini alijibu kwa njia ya ujumbe mfupi kwamba bado  hajapokea taarifa na akaahidi  kufuatilia kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi.

Matukio hayo ya unyanyasaji kwa wanawake yanatokea kipindi hiki ambacho ulimwengu upo kwenye maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia hali inayodhihirisha


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt