asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, December 5, 2016

viijiji 26 chalinze hoi kwa njaa

WAZIRI KILIMO MIFUGO NA UVUVI MHE. DR. CHARLES JOHN TIZEBA.

VIJIJI 26 kati ya 68 vilivyopo katika Jimbo la Chalinze Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, vinakabiliwa na njaa na vinahitaji msaada wa haraka wa chakula.
Uhaba wa chakula ulivikumba vijiji hivyo umetokana na mvua kutoonyesha katika kipindi kirefu na hivyo kusababisha ukame katika maeneo hayo.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe umebaini kuwa mbali ya wananchi wa vijiji hivyo 26 kukosa chakula, pia mifugo wakiwamo zaidi ya ng'ombe 500, wamekufa kwa kukosa malisho kutokana na ukame.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakizungumza kwa nyakati tofauti kufuatia hali hiyo, wameiomba serikali kuwasaidia wananchi hao kwa kuzingatia vijiji ambavyo vina hali mbaya zaidi.

Mmoja wa madiwani hao wa Kata ya Talawanda, Saidi Zikatimu, alisema awali katika tathmini, waliiomba serikali tani 4,000 za msaada wa chakula, lakini walipatiwa tani 200 pekee.

Diwani Zikatimu alisema kuwa kati ya tani 200 za chakula cha msaada walichopokea, tani 180 ni kwa ajili ya kugawanywa bure na tani 20 ni chakula cha kununua kwa wale wenye uwezo ambacho hakikutosheleza.

Alisema kiasi cha chakula kilichotolewa ni kidogo kwa kulinganisha na hali halisi ya tatizo.

Diwani huyo aliongeza kuwa kama serikali iliona umuhimu wa suala hilo kwa mara ya kwanza, basi isaidie kumaliza msaada kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa.

Alizitaja kata ambazo zilikosa msaada huo wa chakula kuwa ni Vigwaza, Bwilingu na Kiwangwa.

Zikatimu alisema Kata za Msoga, Pera na Ubena, zilipata kijiji kimoja kimoja.

Naye Diwani wa kata ya Kimange, Hussein Hading’oka, alieleza kwamba chakula cha msaada kilivifikia vijiji vitatu na viwili vikiwamo vya Pongwe, Mnazi na Kikwazu, vimekosa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Isaack Kama, alithibitisha kuwapo kwa baa la njaa katika baadhi ya vijiji.

Akizungumzia suala la kufa kwa mifugo Ofisa Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Chalinze, Dk. Khama alisema hadi sasa bado hajapata idadi ya mifugo iliokufa kwa kukosa malisho.

Hata hivyo, Dk. Khama alithibitisha kuwa ng'ombe ni wengi na kuwa kwa Ranchi ya Taifa Ruvu ni mifugo 40 wameripotiwa kufa kwa njaa


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt