asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, March 5, 2017

BREAKING NEWS: Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na njaa

BREAKING NEWS: Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na njaa
Makaburi ya watu nje ya kambi ya watu waliohama makwao eneo la Garowe nchini Somalia.
Pichani nia Makaburi ya watu waliofariki nje ya kambi ya watu waliohama makwao.
Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizopita.
Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Siku ya Jumanne Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.
Umoja wa Mataifa una kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.

Wanyama wamekuwa wakifa nchini SomaliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanyama wamekuwa wakifa nchini Somalia

Mataifa mengine ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Karibu watu 260,000 walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.
Watu wengine 220,000 walifariki kutokana na njaa ya mwaka 1992.
Pia njaa imetangazwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ambayo ndiyo ya kwanza kutangazwa tangu ile ya Somalia ya mwaka 2011.

Mataifa mengine ambayo yako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Image captionMataifa mengine ambayo yako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt