asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, March 5, 2017

Kwa nini Juuko alikaa benchi Kotei akacheza kama beki wa kati? Mayanja katoa majibu…


Mechi ya jana kati ya Simba na Mbeya City, alishuhudiwa kiungo James Kotei akicheza katika nafasi ya beki wa kati sambamba na Abdi Banda huku maswali mengi yakiibuka kwamba, kwa nini Juuko Murshid yuko benchi wakati anaweza kucheza vizuri katika nafasi ya beki wa kati.
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja akafafanua kwa nini waliamua kuweka kando Juuko na kumchezesha Kotei katika nafasi ya beki wa kati.
“Tulikuwa tunamtegemea kwa sababu hatukuwa na namna ya kufanya kuweka mtu yoyote, lakini kama mchezaji akaliambia benchi la ufundi hayupo tayari kucheza kwa sababu amekaa muda mrefu bila kufanya mazoezi. Sisi tukawa hatuna nmna hatuwezi kumlazimisha mchezaji wakati ameshasema hayupo tayari tukakubaliana nae akakaa benchi.”
Mechi ya Simba na Yanga  Banda na Kotei walicheza vizuri katika nafasi ya beki wa kati baada ya benchi la ufundi kumtoa Lufunga na baada BoKungu kuondolewa uwanjani kwa kadi nyekundu.
Mayanja anasema, jana tatizo halikuwa kwenye safu ya ulinzi bali wachezaji wa Simba walipoteza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuumaliza mchezo mapema.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt