asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, December 12, 2016

RAISI ALIYEPITA GAMBIA YAHYA JAMES SASA MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI

 Rais Yahya Jammeh akionyesha ishara ya kidole chake baada ya kupiga kura mjini Banjul baada ya kupiga kura yake

Kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh amesema atakwenda mahakamani kupinga kushindwa kwake katika uchaguzi unaoweka kikomo cha utawala wake wa miaka 22.

Awali rais Rais Jammeh alikubali kushindwa baada ya mpinzani wake Adama Barrow kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa wiki iliyopita, lakini baadae alibadilisha kauli yake Ijumaa, akisema ''anakataa kwa ujumla'' matokeo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka akubali kushindwa.

Mitaa ya mji mkuu Banjul iko katika hali ya utulivu huku jeshi likipiga doria mjini humo.

Muungano wa Jammeh -Alliance for Patriotic Reorientation and Construction party Ulitangaza usiku wa Jumamosi , kwamba utawasilisha kesi katika mahakama kuu ya Gambia.

Kwa mujibu wa sheria za Gambia, malalamiko kuhusu matokeo yanaweza kupingwa kisheria katika kipindi cha siku 10 baada ya kupigwa kura.
Wengi wa raia walisherehekea hadharani baada ya Barrow kutangazwa mshindi

Rais mteule Barrow Jumapili alisema kuwa anahofia usalama wake. Aliwahi kumshutumu Bwana Jammeh kwa kukiuka demokrasia kwa kukataa kukabidhi mamlaka.

Bwana Jammeh, ambaye alinyakua mamlaka kwa njia ya mapinduzi mwaka 1994, ameelezea kuweo kwa ''dosari'' katika upigaji kura na anataka uchaguzi urudiwe.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt