asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, December 12, 2016

KITENDAWILI KIPYA CHA NAPE,SIMBA NA UWANJA WA TAIFA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, jana Jumapili alifanya ziara katika Uwanja wa Taifa, Dar kwa ajili ya kuangalia ukarabati unaofanywa na uongozi wa Klabu ya Simba, kisha akatoa siku tatu kuanzia jana wawe wameshakamilisha marekebisho hayo kutokana na kufanya uharibifu wa viti walipocheza na Yanga uwanjani hapo.
Takribani siku 73 zimepita tangu mchezo wa Ligi Kuu Bara uchezwe kati ya Simba na Yanga ambao ulizaa uharibifu mkubwa wa uvunjaji wa viti 1,784 uliofanywa na mashabiki wa Simba hali iliyosababisha serikali kutangaza kuzifungia timu hizo kutumia uwanja huo.
Waziri huyo ambaye alifika uwanjani hapo mapema asubuhi, alianzia ukaguzi katika chumba maalum cha kamera 119 za ulinzi  zilizofungwa uwanjani kabla ya kuingia uwanjani ambapo alitoa agizo kwa kaimu meneja wa uwanja, Julius Mgaya baada ya kushuhudia baadhi ya maeneo yakiwa bado hayajawekwa viti kuwa ndani ya siku tatu wawe wamekamilisha ili apate kukabidhiwa.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mgaya alisema: “Kwa sasa suala la ulinzi lipo vizuri zaidi kutokana na ubora wa kamera zetu 119 za  CCTV  kuwa na uwezo wa kuona popote na kuzoom nje na ndani ya uwanja, pia kwa ndani ukarabati umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufuatia uharibifu uliotokea Oktoba Mosi, mwaka huu na tunatarajia ukarabati huo kukamilika kabla ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kuanza hapo Desemba 17, mwaka huu.
“Licha ya hivyo kuna ukarabati wa milango ya chuma 33 ilikuwa imeharibika na mpaka sasa milango 13 imeshafungwa. Pia mpaka Machi 3, mwakani tutakuwa tumeshamalizia sehemu ya zima moto tukishirikiana na wenzetu raia wa China.”
Naye Nape alisema: “Ukarabati kama mnavyouona unakwenda vizuri, kuna maeneo viti vilivunjwa na Simba lakini pia yapo maeneo viti vililegea ambavyo vyote kwa pamoja vinafanyiwa ukarabati ila niseme jambo moja kuwa tusisubiri hadi Desemba 17, Desemba 13, Jumanne (kesho) nataka kuja kupokea huu uwanja ukiwa umekamilika.”


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt