asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, April 12, 2017

TAZAMA HAPA JINSI INAVYOTIA HURUMA...Kikongwe wa miaka 100 aliwa na fisi


Kikongwe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 100, Asyenepe Laia, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi.

Miaka 100 auawa na fisi

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya fisi hao kumuua, katika tukio lililotokea Alhamisi iliyopita, waliondoka na mwili wake kwenda katika msitu ulioko jirani na eneo analoishi na kula nyama yake.

Mashuhuda hao walisema katika tukio hilo, Asyenepe alikamatwa na fisi hao alipokuwa anaokota kuni ajili ya kuchochea katika moto alio kuwa ameuwasha ndani ya nyumba yake.

Walisema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kalulu Mashambani kandokando na Hifadhi ya Msitu Hifadhi ya Taifa ya Selous katika Tarafa ya Matemanga, Tunduru mkoani Ruvuma.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Dk. Gaufrid Mvile, alisema chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na kitendo cha wanyama hao kumshambulia.

Alisema katika tukio hilo walikuta mabaki ya vipande viwili vya mifupa, michirizi ya damu na mabaki ya nguo, mambo yaliyoashiria kuwa kikongwe huyo aliuawa na fisi hao na kumla nyama yake yote.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt