asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, September 5, 2017

CCM NDIO KWANZA KUMEKUCHA...!!! POLE POLE APASUKA HADHARANI JUU YA RAIS MAGUFULI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ameshangazwa na raia wa Namibia kwa kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John P Magufuli  kila sehemu nchini humo huku akisema kuwa ni sifa kwa taifa letu.

  Polepole ambaye yupo nchini Namibia kikazi kwa mujibu wa maelezo yake amesema kila mtu anayekutana nae nchini humo anamuulizia Rais Magufuli.

“Niko Namibia kwa kazi ya CCM na kila mtu anamuulizia Magufuli, Magufuli, Magufuli. Huyu Magufuli amerudisha maradufu heshima ya Taifa letu”,ameandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Twitter.

 Humphrey Polepole ni moja ya viongozi wa CCM ambao wanasiasa wengi wanadai kuwa nafasi aliyopewa kwenye chama hicho ni kubwa kulinganisha na uwezo wake akiwemo  Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
TOA MAONI YAKO


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt