Wakili
wa kujitegemea, Hashimu Rungwe amejitokeza kumtetea mfanyabiashara
maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani Hussein maarufu kama
‘Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe’.
Rungwe
aliyekuwa mgombea urais kupitia Chaumma katika Uchaguzi Mkuu uliopita,
alijitokeza jana na kujitambulisha mahakamani kuwa ndiye atamtetea
mshitakiwa huyo.
Ndama
mtoto wa ng’ombe (44) anakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kutakatisha
fedha na kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia ya udanganyifu.
Baada
ya kujitambulisha mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa, Wakili
wa Serikali, Christopher Msigwa alisema kesi hiyo imepangwa kutajwa,
upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine. Hakimu
Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 27,2016.
Mshtakiwa
huyo alipelekwa rumande kwa sababu miongoni mwa mashtaka yanayomkabili
limo shtaka la kutakatisha fedha ambalo halina dhamana.
Katika
kesi hiyo, Ndama anadaiwa kuwa Februari 20,2014 jijini Dar es Salaam,
alighushi kibali cha kusafirisha madini kuonyesha kuwa kampuni ya Muru
Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha kilo
207 za dhahabu yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kwenda
Australia wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kuwa Machi 6, 2014 jijini Dar es Salaam alitengeneza
kibali cha Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonyesha
dhahabu hiyo kutoka Congo inatarajiwa kusafirishwa kwenda Australia.
No comments:
Post a Comment