Goli alilofunga jana wakati Yanga ikicheza dhidi ya Ruvu Shooting, linamfanya Simon Msuva kufikisha magoli 12 kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu na kuongoza kwenye orodha ya wafumania nyavu kwa msimu huu 2016/17 zikiwa zimesalia mechi saba (7) ligi kumalizika.
Msuva alifunga kwa mkwaju wa penati kwenye mechi ya pili mfululizo zikiwa zimepita siku nne baada ya kufunga kwa penati kwenye mechi ya watani wa jadi (Simba na Yanga) mechiiliyochezwa Jumamosi iliyopita (February 25, 2017) na kumalizika kwa Yanga kufungwa 2-1.
Kwenye orodha ya wachezaji saba wenye magoli mengi kwenye ligi msimu huu, Yanga inawachezaji wanne kwenye orodha hiyo hivyo inaashiria ni namna gani kikosi hicho kilivyo na wachezaji wenye njaa ya kutupia kambani.
Kati ya wafungaji saba wenye magoli mengi hadi, wafungaji wanne ni wazawa huku wachezaji watatu wakiwa ni wakigeni. Msuva, Kichuya, Bocco na Mbaraka Yusuph wote ni wachezaji wa kitanzania wenye magoli mengi hadi sasa kwenye ligi lakini Tambwe, Ngoma n a Chirwa wote kutoka Yanga wao ni wachezaji wa kigeni wenye magoli mengi kwenye ligi msimu huu.
Licha ya kuwa na wachezaji wa kimataifa kwenye nafasi za ushambuliaji, vilabu vya Simba na Azam bado wafungaji wake wenye magoli mengi ni wa zawa huku kila klabu (kati ya vilabu hivyo viwili) ikitoa mfungaji mmoja kwenye orodha ya wafungaji.
Kagera Sugar ndio timu pekee ambayo haina jina kubwa kwenye msimamo wa ligi iliyotoa mfungaji kwenye orodha ya watupiaji msimu huu, Mbaraka Yusuph mwenye magoli nane anaungana na wachezaji kutoka Simba, Yanga na Azam kwenye orodha ya wanaowania ufungaji bora msimu huu
No comments:
Post a Comment