Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa amesema
kuwa aliyekuwa Rais wa Cuba na mwana mapinduzi wa nchi hiyo, Fidel
Castro alimhamasisha kuingia katika uongozi.
Ameyasema
hayo alipotembelea ubalozi wa Cuba hapa nchini kutoa pole na kusaini
kitabu cha maombolezo ya kifo cha Castro kilichotokea Novemba 25 mwaka
huu jijini Havana nchini Cuba.
Lowassa
amesema Marehemu Castro alikuwa mwana mapinduzi na ni miongoni mwa
wanasiasa waliomhamasisha kuingia kwenye uongozi kutokana na alivyokuwa
akiwatetea masikini na wanyonge duniani, hali ambayo imelisababishia
taifa hilo dogo kuogopwa kutokana na uimara wake.
“Castro
alikuwa kiongozi imara sana,kila kiongozi makini lazima awe kinara wa
kuwatetea wanyonge na masikini popote walipo”alisema Lowassa.
Lowassa
amesema kuwa Castro aliifanya Cuba pamoja na udongo wake uitikise dunia
kwa kuwa kila mahali ukienda ni lazima utasikia jina la Castro.
No comments:
Post a Comment