Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Pius Maneno
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imepitisha
na kutangaza matokeo ya watahiniwa 6,282 waliofanya mtihani kati ya
Novemba mosi hadi 4 mwaka huu katika ngazi mbalimbali za masomo, huku
watahiniwa 2,898 wakishindwa kabisa katika mitihani yao.
Katika matokeo hayo, watahiniwa waliokuwa wamejisajili kufanya mitihani
ni 6,917 ambapo kati yao watahiniwa 653 (asilimia 9.2), hawakufanya
mitihani hiyo kutokana na sababu mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Pius Maneno,
ilieleza kuwa matokeo hayo yanafuatia mitihani iliyofanyika katika vituo
11 vya mitihani kutoka mikoa kadhaa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Mitihani hiyo ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya pili
katika ngazi ya cheti cha utunzaji wa Hesabu (ATEC I, ATEC II) zenye
masomo manne kila moja na ngazi ya taaluma, Hatua ya awali/msingi yenye
masomo matano, Hatua ya Kati yenye masomo sita na hatua ya mwisho yenye
masomo manne.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa watahiniwa 263, kati ya 6,282, waliofanya
mitihani hiyo, wamefaulu huku wengine 281 (4.4%) wakifaulu katika
mitihani yao waliyokuwa wameshindwa awali. Pamoja na ufaulu huo,
watahiniwa 2,119 wameshindwa katika baadhi ya masomo yao huku 2,898
wakishindwa mitihani yao.
No comments:
Post a Comment