Jamii ya hip hop nchini Tanzania imegawanyika katika matababa mawili.
La kwanza ni la wale wanaosema wanazingatia misingi ya hip hop na wale
ambao wanafanya ile wanayoiita hip hop ya biashara.
Tabaka la kwanza, linaaamini kuwa hilo tabaka la pili limekiuka
misingi ya hip hop wanayoiamini na kwamba halipaswi kusema linafanya
muziki huo. Mdahalo ni mzito na mara nyingi huhusisha hisia kali ambazo
huibua hasira.
Mmoja wa wasanii w tabaka la pili ambao amekuwa shabaha ya kejeli na
matusi kutoka kwa tabaka la kwanza ni Nay wa Mitego ambaye anadai kuwa
hao wanaosema hafanyi hip hop hawana lolote.
“Hao wanaosema mimi sio mwana hip hop nipeleke nao kwenye show moja,
hao walionitoa kwenye list ya hip hop. Tena ninachokuomba waandalie show
yao Leaders waweke 16, niandalie show yangu Escape 1 peke yangu.
Nakuambia wakipata watu kweli hip hop yao ina nguvu. Wote unaowasikiaga
waandika, wanakesha, wanatweet ‘Nay si mwanahiphop’ wajikusanye kwenye
show yao moja halafu mimi nipige pale upande wa pili halafu tuone nani
atapata watu,” Nay aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Wewe unakesha unanitukana kwenye mtandao wakati mimi nikiamua
asubuhi naenda kununua gari mpya, nikiamua naenda kununua kibanda chenu
kile cha familia mimi ninakinunua halafu wewe unaenda kukaa unanitukana
kwenye mitandao, siwezi kukasirika,” amesisitiza.
Nay anaamini kuwa kama kila msanii atapata fedha kwa muziki anaofanya hakutakuwa na chuki kama anayoiona dhidi yake kwa sasa
SLIDE MANENO
Friday, December 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment