asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Saturday, December 3, 2016

sasa NEC yapata ugeni wa dunia

NEC yapata ugeni wa dunia

UJUMBE kutoka Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) umeitembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kujifunza hatua mbalimbali zinazofanywa na NEC wakati wa uchaguzi nchini.

Aidha, ujumbe huo umekuja na aina mpya ya teknolojia ambayo ina uwezo wa kuandikisha wapiga kura, kutuma taarifa za wapiga kura katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na kuhakiki wapiga kura siku ya uchaguzi.

Mashine hiyo ambayo ni ndogo ukilinganisha na ile ya Biometric Voter Registration (BVR) ina uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja ambaye ataweza kuandikisha mpiga kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpigakura na inabebeka kirahisi.

Teknolojia hiyo mpya pia inaweza kurahisisha utendaji kazi katika masuala ya uandikishaji wapiga kura, kuhakiki wapiga kura na kutuma taarifa katika kanzidata.

Ujumbe wa AWEB kwa NEC umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi, Park Jae Sumg.

Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo, kutembelea ofisi mbalimbali za tume hiyo na kujifunza.

Akizungumzia ujio wao jana jijini Dar es Salaam, Ju-Hwan alisema yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika teknolojia ya kuandikisha wapiga kura.

Wakiwa katika kikao na baadhi ya watendaji wa NEC, ujumbe ulipata nafasi ya kujifunza BVR zinavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyoweza kuandikisha wapiga kura wengi kwa kutumia mashine hiyo na changamoto zake.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt