Kufuatia malalamiko ya wakina mama wajawazito katika hospitali ya wilaya
ya Nzega na vituo vya Afya kulalamikia tabia ya wauguzi na madaktari
kuwatoza fedha wakati wanapoenda kujifungua Mkuu wa mkoa wa Tabora
AGGREY MWANRY amemuagiza mkurugenzi na mganga mkuu wa wilaya ya Nzega
kusimamia na kuhakikisha wakina mama hao wanarudishiwa fedha zao zote
walizotozwa.
Kwa mujibu wa sera ya Afya ya Taifa wakina mama wajawazito wanapaswa
kupatiwa huduma za matibabu bure lakini hali imekuwa tofauti katika
hospital ya wilaya ya Nzega ambapo wakina mama hawa wamekuwa
wakilazimika kulipia gharama za matibabu na hapa wanaleta kilio chao kwa
mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya kufanya ziara katika hospitali ya
wilaya ya hiyo
No comments:
Post a Comment