Chadema imeamua kuja na mpango mpya wa kuhakikisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatolewa mahabusu.
Lema
amekuwa mahabusu tangu Novemba mwaka jana, lakini chama hicho kimesema
sasa kinataka apate haki ya kisheria na kuwa huru kwa kuwatumia
wanansheria katika kesi mbalimbali zinazomkabili.
Mwanasheria
Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema hayo baada ya yeye, mwenyekiti
wake, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine kumtembelea Lema mahabusu
anakoshikiliwa tangu Novemba 2, mwaka jana kwa tuhuma za kutoa lugha za
uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.
Lema
amekuwa akikwama kupata dhamana kutokana na sarakasi za kisheria
zilizosababisha upande wa utetezi uende hadi Mahakama Kuu katika
kuhakikisha anapata haki hiyo, lakini hadi sasa bado vita hiyo ya
kisheria haijaisha.
Lissu
amewaambia waandishi wa habari mjini Arusha kwamba wataongeza nguvu ya
mawakili wa Chadema katika kesi hiyo kila itakapokuwa ikitajwa
mahakamani.
Pia,
watakiandikia Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) barua rasmi
kukitaka kitoe tamko kwa namna yoyote ili kiseme katika kesi ya Lema
kipo upande upi na kama kikisema hakihusiki, basi hakutakuwa na chama
cha wanasheria nchini na wakiona kuna hoja, basi watawataka watoe
mawakili waliopo Arusha kusaidia kesi zinazomkabili Lema.
“Hawa
wanasheria wasijidai hamnazo wakati mbunge wao yupo mahabusu.
Tutawaambia wawepo mahakamani kwa kuwa wananchi wa kawaida hawaruhusiwi
kuja kusikiliza kesi hiyo, basi wajae wanasheria,” amesema Lissu.
Awali,
Mbowe amesema chama na viongozi waliamua kwenda kumuona Lema na familia
yake kwa kuwa yupo mahabusu kinyume na haki za binadamu.
“Lema
ana moyo mkuu sana na amejifunza mambo mengi kwa mujibu wa maelezo
yake. Anasema wapo mahabusu asilimia 70 wenye makosa yanayostahili
kupewa dhamana, lakini hawajapewa,” amesema.
No comments:
Post a Comment