Je unawazo la kuanzisha biashara yako, lakini hujui aina ya biashara
itakayokutoa kimaisha? hapa chini kunanjia muhuimu zitakazokusaidia ili
uweze kuanzisha biashara yako ndogo itakayokuwezesha kusonga mbele
kimaisha.
Huenda ukawa umegundua kuwa kuna mawazo au aina milioni moja za
biashara, lakini ukachagua wazo moja tu, ambalo hilo utakuwa umefanya
maamuzi magumu na yapekee kulipa kipaumbele. Japokuwa haina haja ya
kulipa kipaumbele wazo moja tu na kuliona ndilo la pekee katika kuanza
biashara yako ndogo.
Wazo lolote lile la biashara ulilochagua, ningependa kukushauri kuwa
usianzishe biashara ambayo ni maarufu kwa wakati huo, biashara ambayo
inafanywa kwa kiasi kikubwa na wafanya biashara walio wengi. Ukifanya
hivyo utawanufaisha wafanya biashara wakubwa kwanza halafu wewe utakuwa
wa mwisho. Hapo chini ni mbinu au njia chache zitakazokusaidia ili
uchague wazo (idea) zuri la kuanzisha biashara yako ndogo.
Wazo lako la kuanzisha biashara yako, ni lazima litokane na sehemu ya
shughuli zako ambazo tayari ni sehemu ya maisha yako, shughuli mbazo
tayari unazifurahia kuzifanya kila kukicha. Unapaswa kufanya kitu
unachokipenda kutoka moyoni, kitu ambacho kinakufurahisha kila kukicha.
Kwa mfano, mimi mwenyewe tofauti na kazi yangu, tumechukua muda na
kutengeneza blog hii, kwasababu hutufanya tujisikie wenyefuraha
tunapoifungua kila siku na kuandika kitu kikasomwa na watu wengi sana
kwa siku.
Pia unatakiwa kujifunza mengi zaidi kuhusiana na wazo lako la biashara
uliloliteua. Lifanyie utafiti wakutosha, kwani unavyozidi kujifunza
mengi, ndivyo unazidi kuwa mzoefu katika kuanzisha biashara yako.
Ukifanya hivyo utaanza biashara yako ukiwa na uzoefu wa hali ya juu na
mafanikio yatakuwa upande wako siku zote.
Kitu muhimu: Wazo lako la kuanzisha biashara lazima liendane na
mahitaji ya wateja au wanunuzi. Endapo kama haliendani au kukidhi
mahitaji ya watu, basi hakuna mtu atakaye kuja kununua bidhaa yako au
huduma yako. Hivyo fanya kwanza utafiti kabla ya kuanza. Hakikisha
unafanya utafiti wa mahitaji ya wateja, hata ikiwezekana waulize watu wa
eneo hilo mahitaji wanayohitaji kununua ndipo uanzishe biashara yako.
Mwisho kabisa, katika dunia hii asikwambie mtu, biashara ni matangazo,
bila matangazo ni sawa na bidhaa bila mnunuzi. Fanya hima tangaza
biashara yako katika vyombo mbali mbali vya habari, utaona manufaa ya
kazi yako
SLIDE MANENO
Wednesday, January 4, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment