Shirika la utangazaji nchini Tanzania TBC, limewasimamisha kazi wafanyakazi tisa baada ya taarifa za uongo kuwa Rais wa Marekani Donald Trump, alimpongeza rais John Magufuli, kupeperuswa hewani.
Taarifa hizo zilizopeperushwa wiki iliyopita zilisema kuwa Trump alitoa wito kwa viongozi wengine wa Afrika kufuata mfano wa Magufuli kwa uongozi bora na kupambana na haswa na ufisadi.
"Makosa hayo hayangefanyika ikiwa taratibu za uhariri zingefuatwa," Mkurugenzi mkuu wa TBC Ayub Chacha alismea.
Makala hiyo bandia ilichapishwa kwenye wavuti wa "Fox Channel" ambayo hutoa taarifa zake kutoka kwa mitandao mingine.
Taarifa hiyo ya uongo inasema kuwa Trump alimtaja magufulia kama "shujaa wa Afrika", wakati akiweka sahihi sheria ya kuwazuia waafrika kutoka nchi ambazo marais hawafanyi lolote pamoja na wale wamekatalia madarakani.
Raia wa Tanzania hawatazuiwa kuingia Marakani, taarifa hizo zilisema.
source:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment