asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, March 19, 2017

HATARI!!!: MAGUFULI KUADHIBIWA KWA MGONGO WA MAKONDA

Image result for MAGUFULI


Kwa takribani mwezi sasa, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndiye amekuwa akivuma (trend) katika vijiwe vingi vya watanzania mitandaoni, kwa sababu mbalimbali. Nyingi ya sababu zinazomvumisha, ni tuhuma za uhalifu na maadili. Japo tuhuma zenyewe hazijathibitishwa na vyombo husika, zina chembe chembe nyingi mno zinazoashiria uhalali wake, yakiwemo matendo ya mtuhumiwa.
Kwa hali ilipofika sasa, itakuwa vigumu sana kwa Mh Rais na serikali yake kuendelea kupuuzia hizi tuhuma. Ni lazima zifanyiwe uchunguzi, na zikithibitika kuwa ni za kweli, basi hatua zichukuliwe dhidi ya mhusika. Hapa ndipo inapokuja hoja yangu kuwa Mh Rais pia atastahili kuwajibika pia, endapo Makonda atapatikana na hatia.

Nasema Rais pia awajibike kwa sababu;

Moja, Mh Rais alimu-endorse Makonda, na alimpa baraka na ushirikiano katika utendaji wake wa kila siku, ikiwemo vita dhidi ya madawa ya kulevya ambayo inahusika katika moja ya tuhuma nzito zinazomkabili Makonda. Kitendo cha Rais kumuunga mkono Makonda kinaashiria mambo mawili; aidha walishiriki pamoja katika uchafu huo, au Mh Rais alimuamini tu Makonda pasipo kufanya uchunguzi ambapo kutamaanisha kukosa umakini katika utendaji, either way Mh Rais atapaswa kuwajibika.

Mbili, Kitendo cha Mh Rais kupuuzia ku-address hizi tuhuma kwa muda mrefu kinanifanya nijiulize mambo mawili; Pengine Mh Rais alizifanyia uchunguzi hizo tuhuma kimya kimya na kujiridhisha kuwa si za kweli, ama anafahamu fika kuwa ni za kweli na kaamua kuzifumbia macho ili kumlinda Makonda kwa sababu moja ama nyingine, ether way Mh Rais anapaswa kuwajibika.

Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni kuwa, tuweke uzalendo mbele ya siasa na hisia zetu binafsi. Hili suala linaiathiri nchi kwa ujumla, bila kujali chama gani cha siasa.

Ni hayo tu.
source:JF


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt