KATIKA kuelekea mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika klabu ya Yanga itawakosa washambuliaji wake wa kutumainiwa Mrundi Amis Tambwe na Donald Ngoma,ambao wote ni majeruhi.
Charles Boniface Mkwasa alisema pamoja na wawili hao ambao ni majeruhi, pia klabu itawakosa kipa Beno Kakolanya, beki Pato Ngonyani, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji wengine wawili, wote wazawa, Malimi Busungu na Matheo Anthony ambao pia ni wagonjwa.
Hiki ndio kikosi kikosi kimeondoka kuelekea Zambia na kitakua na wachezaji 20.
Wachezaji hao ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali, Hassan Kessy, Juma Abdul, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Wengine ni pamoja na Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emanuel Martin.
Yanga inahitaji ushindi wa ugenini Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment