Belle 9 ameitaka serikali kufuta huduma ya PF3 ambayo inaonekana kuchelewesha wagonjwa wengi kuikosa huduma muhimu ya kiafya, inayoweza kuokoa maisha ya watu ndani ya wakati mwafaka.
Muimbaji huyo amesema hayo baada ya kuenea kwa taarifa zinazodai kuwa kifo cha baba yake mzazi, aliyepata ajali usiku wa kuamkia Jumatatu, baada ya kugongwa na pikipiki, kilitokana na kucheleweshwa kupata huduma hospitalini, kutokana na kukosa PF3.
“Mimi nadhani PF3 ingefutwa. Wangebadilisha utaratibu PF3 zitoke baada ya mtu kupata huduma ya kiafya. Kwa sababu mtu anapokuwa amepata ajali katika hali ya kawaida, anakuwa anahitaji huduma haraka, sidhani kama ni PF3 ni important sana kuliko huduma ya kiafya,” Belle amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Ijapokuwa kifo kinapotokea huwezi kukiepuka, tunaweza kutengeneza tu utaratibu ambao labda tunaweza tukapunguza vifo, hata mtu anapopata ajali, anajua anaweza akapata huduma on time,” ameongeza
No comments:
Post a Comment