Aliyekua kamanda wa kikosi cha ulinzi wa Rais amehukumiwa miaka 18 gerezani kutokana na mauaji ya mwaka 2011.
Brunot Dogbo Ble(Republican Guards), nchini Ivory Coast na wengine tisa walipatikana na hatia ya utekaji nyara na mauaji ya wanaume wanne wakiwemo raia wawili wa Ufaransa katika hoteli moja mjini Abdijan.
Utekaji nyara huo ulifanyika wiki za mwisho za vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilizuka baada ya Laurent Gbagbo kung’angania madaraka licha ya kushindwa katika uchaguzi wa Urais mwaka wa 2010.
Aliyekua mkuu wa Polisi wakati huo Osee Longuey alihukumiwa miaka 20 jela.
Wanajeshi wengine wanne wa zamani walipata hukumu ya chini.
Kuna wengine ambao walipatikana bila makosa.
Taarifa zinasema mkuu huyo wa kikosi cha Ulinzi wa Rais aliwateka waathiriwa wake na kuwapeleka katika ikulu ya Rais ambapo waliteswa na kuuawa.
No comments:
Post a Comment