Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao, ili kufikia malengo walioyanayo nchini.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa masuala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni, tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia,”alisema Waziri Ummy.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE, Profesa William Anangisye amesema lengo la mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
No comments:
Post a Comment