Baada ya Paul Makonda hali yake kisiasa kuchafuka kutokana na matendo yake hivi karibuni alikuja Mwanza na kubaini kuwa kwa sasa amepoteza mvuto Kabisa kutokana na kukosa kiki kwenye vyombo vya habari na baadhi ya marafiki zake kuanza kumkimbia.
Inasemekana ujio wa Makonda Mwanza ilikuwa ni Kwa ajili ya kuweka mambo sawa na Mkurugenzi wa Star Tv ndugu Antony Dialo, ambaye walikutana Kwa siri na Mkurugenzi huyo.
Imebainika kuwa Makonda alikuja Kwa malengo matatu la kwanza ni kujaribu kuweka mambo sawa na Dialo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama mkoa wa Mwanza ambaye anaunga mkono tamko la Jukwaa la wahariri kutokurusha habari za Makonda.
Imefahamika katika lengo la kwanza walimtisha mzee Dialo kama atashindwa kufanya kazi pamoja na Makonda watamuondoa mara moja ndani ya chama Kwa kumvua nyadhifa zote za uongozi.
Jambo la pili tulilodokezwa ni kwamba Hali ya uchumi ni mbaya katika kampuni ya Sahara iliyopelekea MD wake ndugu Sammy Nyala kuondoka kutokana kushuka sana kibiashara katika kampuni hiyo inayomilikiwa na Mzee Dialo siku hizi hawafanyi vizuri kibiashara na ukichangia na Deni la zaidi ya shilingi bilioni nne kutoka TRA.
Makonda alimuhaidi atamsaidia kuongea na mamlaka za juu kumpatia TAX HOLIDAY endapo atakubali kufanya naye kazi na kurusha taarifa zake Yeye Makonda.
Makonda katika safari ya Mwanza aliambatana na Ray pamoja JB ambaye hivi karibuni amemteua kuwa mhamasishaji wa wasanii katika kusambaza taarifa za Makonda mitandaoni.
Katika Siku ya Pili pale Malaika Resort Makonda alisikika akiongea kwenye simu na mtu ambaye alionekana kumtii sana ndani ya chama na kumpatia taarifa juu ya adhima ya Antony Dialo kuifikiria zaidi nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Jioni walipokutana Katika hotel ya Malaika Resort Majira ya Jioni Gari ya mzee Dialo ilifika, Makonda na Dialo walizungumza tena Kwa kirefu na kupanga jinsi gani wataweza kufanya kazi pamoja mojawapo ni kujisafisha kuhusu uvamizi wa Clouds Media ili kuizima ishu ya Uvamizi mipango ipangwe haikuwa ishu ya Gwajima bali tetesi za uwepo wa Dawa za kulevya rejea tamko aliloliandika Mzee Dialo.
Pia wakati wanazungumza na Mzee Dialo, Makonda alimjulisha kuwa tayari mipango ya kumuandalia nafasi ya Ukatibu mkuu ndani ya chama CCM Taifa imekwishaiva hivyo asiwe na wasiwasi pale Mkutano Mkuu Taifa utakapoitishwa muda wowote kuanzia sasa kumjadili Nape Nnauye basi ndiyo utakuwa muda muafaka wa jambo lake kuingizwa kwenye ajenda ya Mkutano Mkuu.
Chanzo kilidokeza kuwa Makonda alimuhaidi kumpatia Dialo Kiasi cha fedha ambacho atachukua kutoka kwa Wafanyabiashara marafiki zake wa Dar kwa ajili ya kumsaidia kulipa madeni na Mishahara kwa wafanyakazi wake Kwa mwezi wa 3 hadi wa 6 kwani inasemeka wafanyakazi hao wengi wao bado hawajalipwa Mishahara yao isipokuwa posho ndogo zilizopo Kwa ajili ya kujikimu kwa kuwa hali ya Uchumi kwenye kampuni hiyo ni Mbaya sana.
Kingine Makonda amehaidi kumsaidia Anthony Dialo kwa kumpatia ulinzi kwa kipindi Chote watakachokuwa wanafanya kazi pamoja kumlinda na hasira kutoka Kwa waandishi wasio unga mkono harakati za Makonda.
Baada ya kumaliza Maongezi na na Makonda inasemekana Dialo aliwaita wafanyakazi wake na kujadiliana wajipange jinsi gani ya kufanya kazi na Makonda kitu ambacho Wafanyakazi wametafsiri kuwa ni ishara mbaya kwa kituo hicho cha habari hasa ikichangiwa na uhusiano mbovu na dharau alizozionyesha Makonda kipindi cha nyuma kwa wafanyakazi wa kituo hicho.
Unaambiwa Baada ya Antony Dialo kumaliza kile kikao aliwashinikiza wafanyakazi wake kuwa asiyetaka aondoke akatafute kazi sehemu nyingine Kwa kuwa tayari ajenda pekee alizobaki nazo kwa siri kichwani ni Ukatibu Mkuu wa chama na kusamehewa madeni anayodaiwa.
Kwa Taarifa zilizopo mzee Dialo alikwenda South Africa haijulikani alikwenda kufanya nini, nitaendelea kuwajuza kwa kadri iwezekanavyo juu ya ziara hiyo na kila kitu kitakuwa wazi.
Hii sasa ni kufuru kama Paul Makonda ataendelea kutumia ukaribu wake na Mamlaka za juu ili tu aendelee kujinufaisha Kwa maslahi yake binafsi.
Chanzo - JF
Chanzo - JF
No comments:
Post a Comment