ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wasaidizi wake watatu wanaotuhumiwa kushindwa kuhifadhi silaha na risasi wanatarajiwa kuhukumiwa Julai 31, mwaka huu.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, baada ya jana wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa wamefunga ushahidi wao wa mashahidi sita.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha alisema anaahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, mwaka huu kwa ajili ya kusoma hukumu.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Shedrack Kimaro na Joseph Maugo.
No comments:
Post a Comment