Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwingulu Nchemba amewachana wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.
Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache.
Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba.
Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini mikataba mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini.
“Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa ikiwemo ya makampuni ya madini, haikuwa sawa… Ndio maana imelalamikiwa kwa muda mrefu,” alifafanua Mwigulu.
No comments:
Post a Comment