SLIDE MANENO
Friday, June 9, 2017
SI CCM SI ACT-WAZALENDO ANNA MGHIRA AAMUA KUNG'ATA HUKU NA HUKO, TAZAMA HAPA MCHEZO MTATA ANAOUCHEZA
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira emepinga kuvuliwa uenyekiti wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo na Baraza la Uongozi juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana muda mfupi baada ya kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa mara ya kwanza na kupokelewa na watumishi wa 'bomani', Mghwira alisema Baraza la Uongozi halina mamlaka ya kumuondoa kwenye nafasi mwenyekiti wa chama.
Aidha, alisema chama hicho kilifanya maamuzi ya haraka.
Alisema wakati waliomvua madaraka ni Baraza Kuu la Chama, mamlaka ya kumpumzisha mwenyekiti kwenye nafasi yake yamekasimiwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa mujibu wa katiba ya ACT-Wazalendo.
“Niliwasiliana na muasisi wa chama ambaye ni mheshimiwa Zitto Kabwe kwa ujumbe wa simu kwamba nilikuwa kwenye pilika pilika za kuapishwa, hivyo nilimtaka asubiri hadi Juni 15 mwaka huu ambapo ningekutana nao kwenye Mkutano Mkuu wa chama," alisema mama Anna.
"Lakini baraza limeamua kufanya maamuzi ya haraka.”
Alisema hata Rais John Magufuli ni mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini pia anatumikia nafasi yake ya urais.
Mama Anna, ambaye anakuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuteuliwa kuongoza mkoa katika historia ya nchi, alisema uamuzi wa Baraza la Uongozi umempunguzia majukumu, hata hivyo.
Aidha, mama Anna alisema nia yake ni kuwatumikia wananchi na kuchochea maendeleo.
Alisema Rais Magufuli aliona yeye ni mwanasiasa mzuri na ndiyo maana akaamua kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ili awatumikie wananchi.
Mghwira aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Jumamosi iliyopita na kuapishwa Jumanne, kuchukua nafasi ya Said Mecki Sadiki aliyemwandikia Rais barua ya kuomba kupumzika.
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment