asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, January 29, 2018

RASMI: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017-2018 HAYA HAPA

Matokeo ya kidato cha nne 2017-2018 haya hapa
Image result for matokeo kidato cha nne
Kutazama matokeo bofya HAPA>>>>
Read more »


Thursday, January 4, 2018

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIA KUFANYA MAANGAMIZI LEO, NDANI NI MAJEMBE TUPU JIONEE MWENYEWE



LINE UP - SIMBA SC
04.01.2018.

1.Emanuel Mseja- 30
2.Erasto Nyoni- 18
3.Shiza Kichuya- 25
4.Juuko Murshid-06
5 Asante Kwasi- 16
6.James Kotei - 03
7.Nicholas Gyan- 29
8. Yassin Mzamiru-19
9.Moses Kitandu - 35
10.John Bocco-22
11.Mwinyi Kazimoto -24

SUBS.
1. Ally Salim- 31
2.Jonas Mkude - 20
3.Said Hamisi -13
4.Yusufu Mlipili-05
5.Jamal Mwambeleko -26
6.Mohamed Ibrahim-04
7.Kelvin Faru - 40
8.Laudit Mavugo -11.
Read more »


MAGUFULI AAMUA KUWEKA GRISI KWENYE VYUMA VYA UCHUMI

Image result for magufuli
Leo Ikulu jijini Rais Magufuli alimuaga gavana anayemaliza madaraka yake, Beno Ndulu na kumkaribisha Luoga. Baada ya maagano amesema amepanga kuanzia mwezi ujao kulipa madeni ya ndani ikiwemo ma-suppliers wa chakula kwenye shule na vyuo pia contractors kwani kwa sasa uchumi unaenda vizuri sana na kuna pesa nyingi.

Rais Magufuli pia amesema yapo madeni ya wafanyakazi kama walimu na kutaka madeni yote ya wananchi yalipwe na atatoa bilioni 200 zikalipe. Amedai angeweza kutoa hata kesho lakini uhakiki upite kwanza na wakimaliza mapema amemruhusu gavana azitoe.

Amesema anaamini zitawasaidia wananchi kwa sababu bilioni 200 sio kitu kidogo kuzitoa kwa pamoja na wadeni wote wa ndani wanaoidai serikali walipwe.

Magufuli amesema anaamini magavana watakubaliana nae hio ni njia mojawapo ya kuboost(Kuhuisha) uchumi kwani bilioni 200 zinazotolewa zitasambaa kwa wananchi na gavana anaechukua madaraka alisimamie vizuri.

Read more »


Tuesday, September 5, 2017

KIMENUKA..!!! MECHI YA SIMBA NA AZAM KUCHEZEWA UWANJA WA AZAM COMPLEX NI KIZUNGUMKUTI




Mashabiki wa soka wamelalamika kitendo cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC kupelekwa Azam Complex, Chamazi.

TFF imeamua kutangaza michezo ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC, sasa nayo itakuwa inachezwa Azam Complex tofauti na awali kutokana na ukubwa wake ilitakiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa au ule wa Uhuru. 

Safari hii, Azam FC itaikaribisha Simba Chamazi katika mechi itakayopigwa Jumamosi ikiwa ni ya pili ya Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kila timu.
Mashabiki hao walioandika maoni katika mitandao ya Kijamii ya Salehjembe pamoja na blog yenye ya Salehjembe wamelia kutotendewa haki.

Kwa ujumla mashabiki hao wamelalamika kuhusiana na udogo wa uwanja wa Azam Complex wenye uwezo wa kuchukua watu 7,000.

“Nafikiri hii si sawa, wote tunajua uwanja huo ni mdogo na hii ni mechi kubwa. Wanatunyima haki ya kuona mechi hiyo.

“Angalau kungekuwa hakuna viwanja, lakini kuna Uhuru upo pale.”

Wengine walilalamikia umbali wa Chamazi na muda ambao mechi imepangwa Saa 1 usiku.

Lakini Azam FC imekuwa na kilio cha kutaka kucheza mechi zake nyumbani jambo ambalo hatimaye limetimia.
Read more »


CCM NDIO KWANZA KUMEKUCHA...!!! POLE POLE APASUKA HADHARANI JUU YA RAIS MAGUFULI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ameshangazwa na raia wa Namibia kwa kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John P Magufuli  kila sehemu nchini humo huku akisema kuwa ni sifa kwa taifa letu.

  Polepole ambaye yupo nchini Namibia kikazi kwa mujibu wa maelezo yake amesema kila mtu anayekutana nae nchini humo anamuulizia Rais Magufuli.

“Niko Namibia kwa kazi ya CCM na kila mtu anamuulizia Magufuli, Magufuli, Magufuli. Huyu Magufuli amerudisha maradufu heshima ya Taifa letu”,ameandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Twitter.

 Humphrey Polepole ni moja ya viongozi wa CCM ambao wanasiasa wengi wanadai kuwa nafasi aliyopewa kwenye chama hicho ni kubwa kulinganisha na uwezo wake akiwemo  Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
TOA MAONI YAKO
Read more »


Monday, August 7, 2017

UFALME WA DIAMOND WCB UMEVAMIWA, TUSIMALIZE UHONDO VIDEO MBILI HIZI HAPA CHINI RAYVAN AFANYA MAAJABU, JIONEE MWENYEWE

Mwimbaji kutoka WCB Rayvanny amerudi kwenye TV na hii video mpya inaitwa ‘Chuma Ulete’ enjoy dakika 4 na sekunde 48… ukishaitazama hapa chini usisahau kutoa comment yako umeipokeaje. 
usikose pia video hii hapa chini


Read more »


Wednesday, August 2, 2017

VIDEO: HAJI MANARA AIFIKISHA YANGA TFF, JIONEE MWENYEWE HII HAPA

Image result for video play image
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club, Haji Sunday Manara aiomba Shirikisho la soka nchini (TFF) iwaruhusu kuchezesha wachezaji tisa uwanjani badala ya 11 katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga SC.



Manara ameyasemahayo huku akitanabaisha kuwa kipigo chao kwa Yanga hakiepukiki.

“Mchezo wa Yanga na Simba natamani uwekesho kwa sababu inasaidia kupunguza kelele mtaani na maneno ya kuzuazua”.

“Tunawaomba TFF kama wataweza waturuhusu tuanze na wachezaji tisa hivi kama wataturuhusu na kanuni zinaruhusu tutawaandikia barua rasmi ikiwezekana tuanze tisa tutawafunga tu Yanga”

Afisa huyo aliyetoka kifungoni hivi karibuni kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameongeza kuwa ameyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba Omog juu ya kumvua unahodha, Jonas Mkude

“Mimi ukiniambia, kwangu nimefurahia hili kwa sababu ukiwa nahodha unakuwa unabeba vichwa vya wachezaji kumi sasa kutolewa katika unahodha itamsaidia kumrudisha katika kiwango chake zaidi”.
VIDEO:
Read more »


Tuesday, July 25, 2017

IMEVUJA!! SAID NDEMLA SIMBA NDIO HIVYO TENA,,,!!! AAMUA KUTEMBEA JUU YA NYAYO ZA THOMAS ULIMWENGU

Image result for SAID NDEMLA
Safari ya kiungo Said Ndemla kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC ya Sweden imewadia.

Hii ni baada ya klabu ya Simba kutoa ruhusa kwa kiungo huyo kwenda kufanya majaribio.

Mwishoni mwa msimu wa mwaka jana, Simba waligoma Ndemla kwenda kufanya majaribio AFC ya Sweden ambaye anaichezea Thomas Ulimwengu kwa kuwa walikuwa wakimhitaji.

Simba walitoa sababu kwamba walikuwa wakimhitaji Ndemla katika mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara pia Kombe la Shirikisho.

Ingawa uongozi wa Simba umekuwa hautaki kulifafanua suala hilo, taarifa za uhakika zinaeleza Ndemla ameishapata visa na anaweza kuondoka nchini wakati wowote kwenda Sweden.
Read more »


MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt