asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, December 20, 2016

Balozi wa Urusi nchini Uturuki auawa kwa kupigwa risasi hadharani

Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrei Karlov ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa Jumatatu na afisa wa polisi wakati akihutubia kwenye maonesho ya picha mjini Ankara kama kisasi kutokana na ugomvi wa Syria.

Balozi huyo mwenye miaka 62, alipigwa risasi kadhaa na mtu huyo aliyekuwa amesimama nyuma yake huku akipiga kelele, Allahu Akbar, We die in Aleppo, you die here!’ Alisikika akisema pia, ‘Only death will take me out of here.’

Muuaji huyo aliyekuwa amevaa suti na tai, amejulikana kwa jina la Mevlüt Mert Altintas, 22. Alidai kupiga kwanza risasi hewani kabla ya kumlenga balozi huyo.

Baada ya hapo aliwageukia watu wengine waliokuwa hapo na kuwajeruhi watatu kabla ya naye kuuawa na polisi.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amelaani vikali tukio hilo.

Mauaji hayo yamekuja baada ya siku kadhaa za maandamano nchini Uturuki dhidi ya namba Urusi inavyohusika nchini Syria.



No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt