asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, December 2, 2016

Makala: Elimu kwa Kiswahili au Kingereza?

Kipindi nasoma elimu ya Msingi mwisho mwa miaka ya tisini mpaka mwanzon Mwa miaka ya 2000, tulizoea kuziita shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia kama "international school", ni shule ambazo tuliziona kama za watu wa kipekee sana ukilinganisha na shule zetu za kawaida, nilipofika kidato cha kwanza nakumbuka darasani tulikua na mwanafunzi aliyehitimu St marry, ni mwanafunz ambaye alikua active katika masuala mbalimbali  na kutufanya wengine tujione kama "vilaza", kumbe kilichotengeneza tofauti baina yetu sisi na yule mwenzetu ni KUJIAMINI kwake kulikochagizwa na umahiri wake wa lugha hii ya malkia, back to the topic, Leo hii serikali yetu imekuwa na mchakato wa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu hapa nchini, sio suala baya kwa afya ya lugha yetu adhimu ya kiswahili lakini kwa hali halisi ya karne hii je kuna faida kuzalisha wasomi na wataalamu wenye umilisi wa kiswahili pekee? Napata shida kukubaliana na jibu la ndiyo kwenye hilo swali kwa kuzingatia hali halisi ya mtangamano unaoendelea katika ngazi ya ukanda, bara na hata dunia kwa ujumla.. Leo hii ambapo kiingereza ni lugha ya kufundishia kuanzia kidato cha kwanza lakin wahitimu wetu wengi wamekosa umahiri wa lugha ya kiingereza hata kujielezea wao binafsi je itakuaje kiswahili kikishika hatamu?umuhimu wa elimu kwa lugha ya kiingereza unathibitshwa na ongezeko la kasi la shule zinazotoa elimu kwa lugha hyo almaarufu "English medium schools" ni suala lililo wazi kwamba wazazi wengi wanapenda watoto wao wapate elimu kuanzia ngazi za chini mpaka za juu kwa lugha ya kiingereza isipokua watunga sera wetu wanaongozwa na wanasiasa ambao wanatumia lugha ya kiswahili kujiongezea umaarufu ilihali watoto zao wanasoma "english medium schools". 
Elimu kwa kingereza haikwepeki. 


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt