asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, May 29, 2017

SERIKALINI HAKUKALIKI..!!! MCHANGA WA MADINI KAA LA MOTO, BAADA YA KUTUMBULIWA PROF MUHONGO!!! MWIGULU NCHEMBA NAYE KIZUNGUMKUTI..........TAZAMA HAPA KILICHOTOKEA


Waziri   wa Mambo ya Ndani, Mwingulu Nchemba amewachana  wanasheria wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.

Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji Frederick Werema na amewataka wamwache  Rais John Magufuli aendelee kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache.

Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa  na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba.

 Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini  mikataba mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini.

 “Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa ikiwemo ya makampuni ya madini, haikuwa sawa… Ndio maana imelalamikiwa kwa muda mrefu,” alifafanua Mwigulu.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt