asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, December 5, 2016

MKE WA LEMA AZUA MAPYA JUU YA KESI YA MUMEWE

Neema Lema, mke wa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, amesema yeye na watoto wake hawajutii kutokuwa na mwanasiasa huyo ambaye yuko mahabusu kwa kuwa anapigania haki ya kidemokrasia.

Lema, ambaye alikamatwa Novemba 2 mjini Dodoma, hatakuwa pamoja na familia yake msimu huu wa sikukuu baada ya Mahakama Kuu kutupa hoja zake za kupinga kunyimwa dhamana katika kesi inayomkabili ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. Mbunge huyo atakaa mahabusu hadi Januari.

“Mimi na hata watoto wangu, hatusikitiki kumkosa Lema ambaye yupo mahabusu. Tungejisikia vibaya sana kama Lema angekuwa mahabusu kwa kesi kama ya wizi au makosa mengine ya jinai,” alisema Neema


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt