asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Friday, February 24, 2017

KISA CHA WATANZANIA KUTIMULIWA MSUMBIJI CHAWEKWA WAZI.......

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo.

Mahiga amesema kuwa Watanzania hao wamefukuzwa Msumbiji baada ya kubainika kuwa wanaishi nchini humo bila kuwa na pasipoti za kusafiria, vibali vya kuishi na kutofuata vigezo walivyokuwa wamepewa na mamlaka husika ya nchi hiyo.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugeni unaotarajiwa kuwepo nchini Tanzania wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya Kitaifa nchini Februari 25 na 26, 2017.

Rais wa Visiwa va Shelisheli, Mhe. Dannu Faure naye atawasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe 27-28, februari mwaka huu
USIKOSE PIA HABARI HIZI.........



No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt