asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, March 27, 2017

Mbowe aja na msimamo mkali juu ya utawala wa Magufuli....aahidi kujiuzulu siasa usipotekelezeka



MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema Rais Dk. John Magufuli atakuwa kiongozi wa kwanza nchini kuvunja rekodi ya kutawala kwa kipindi cha miaka mitano badala ya 10 kama walivyofanya watangulizi wake, nje ya msimamo huo wa Mbowe, pia ameahidi kujiuzulu siasa kama isipokuwa hivyo 2020.

Mbowe aliyasema hayo jana wakati akizindua tawi la wakereketwa wa chama hicho lililopo eneo la Mpakani, Kata ya Kwakifua, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Katika hoja hiyo, Mbowe alisema Rais Magufuli ataongoza kwa muhula mmoja kwa kuwa utawala wake hauthamini utu wa binadamu, na ikiwa vinginevyo, yuko tayari kuachana na siasa. “Watu wa Tanga mmechelewa sana kuiondoa CCM madarakani, tulifanya makosa kumchagua Rais wa Awamu ya Tano, matokeo yake wote tunaisoma namba. Tunaanza maandalizi mapema, maana huyu rais atatawala miaka mitano na akiendelea naacha siasa,” alisema Mbowe.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt