asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, February 8, 2017

Mohamed Abdullahi Farmajo ashinda urais Somalia

Mohamed Abdullahi Farmajo

Waziri mkuu wa zamani wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo ndiye rais mpya wa Somalia baada ya aliyekuwa rais Hassan Sheikh Mohamud kukubali kushindwa baada ya kumaliza wa pili kwenye duru ya pili ya uchaguzi.
Farmajo alipata kura 184, Bw Hassan Sheikh akapata kura 97 naye rais mwingine wa zamani Sharif Sheikh Ahmed akapata kura 46.
Mshindi alitakiwa kupata thuluthi mbili ya kura zote zilizopigwa lakini kabla ya duru ya tatu kufanyika, Bw Hassan Sheikh alikubali kushindwa na kumpongeza Farmajo.
Farmajo alihudumu kama waziri mkuu nchini Somalia mwaka 2010 na 20
 Huu ni ushindi wa Somalia na kwa Wasomali," Farmajo aliwaambia wabunge waliokusanyika katika ukumbi ulio katika uwanja wa ndege Mogadishu, ambao ndio waliomchagua.
Aliapishwa kura rais muda mfupi baadaye.
Baada ya habari za ushindi wake kuanza kuenea, milio ya risasi ilisikika pande mbalimbali za Mogadishu, watu wakisherehekea ushindi wake.
Mwanamke wa kwanza kutangaza kuwa angewania urais nchini Somalia ingawa alijiondoa baadaye, Fadumo Dayib ameonekana kufurahia ushindi wa Farmajo.
Ameandika kwenye Twitter: "Wabunge bila shaka wamechagua chaguo la wananchi. Wameiokoa Somalia!! Kumepambazuka, ni mwanzo mpya!"
Taifa la Somalia linalokabiliwa na vita vya kikabila pamoja na vile vya ukoo halijafanikiwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia unaoshirikisha raia kushiriki katika uchaguzi tangu 1969.
Uchaguzi huo ulifuatiliwa na mapinduzi, uongozi wa kiimla na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoshirikisha koo na wapiganaji wa al-Shabab.
Uchaguzi huo unaonekana kama mojawapo ya harakati za kujenga tena demokrasia mbali na kuweka uthabiti.

Matokeo ya duru ya kwanza

  • Hassan Sheikh Mohamud - 88 (rais aliyeondoka)
  • Mohamed Abdullahi Mohamed "Farmajo" - 71 (waziri mkuu wa zamani)
  • Sharif Sheikh Ahmed - 49 votes (rais wa zamani aliyemtangulia Hassan Sheikh)
  • Omar Abdirashid A. Sharmarke - 38 (waziri mkuu anayeondoka)


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt