asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Wednesday, February 8, 2017

MANJI AMUWASHIA MAKONDA MOTO WA CHUMA:SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA



Mfanyabiashara Yusufu Manji amesema kuwa atakwenda Kituo cha Polisi kesho kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivyotaka.

Manji amesema kuwa pamoja na kuwa Makonda ametaka wafike Ijumaa yeye atakwenda kesho huku akihoji kuwa inawezekanaje wakaitwa watu 65 kuhojiwa kama hakuna shughuli za kufanya kwa siku nzima.
“Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa. Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kituo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri,” alisema mwenyekiti huyo wa Yangu akizungumza na waandishi mchana wa leo.
Amesema atakwenda polisi lakini pia hilo suala halitaisha hivyohivyo kwani atakwenda naye hadi mwisho


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt