asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Tuesday, February 28, 2017

MSIMBAZI SASA WANG'OA BEKI WA KIMATAIFA

BEKI wa kimataifa wa Uganda Juuko Murshid amewasili Dar kukiongezea nguvu kikosi cha Simba SC kwa mechi zilizobaki za kombe la shirikisho na zile mechi saba za ligi kuu.
Juuko ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia kwa kufiwa na watoto wake watatu (mapacha) akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON nchini Gabon amewasili jana.
Shaffidauda.co.tz imezungumza na meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi amedhibitisha kumpokea Juuko na kumwambia awasili leo Jumatatu kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Polisi baada ya wachezaji wote wa Simba kupewa mapumziko ya siku moja (jana).
Kurudi kwa Juuko kunaweza kuwa faraja kwa wanachama na wapenzi wa Simba kutokana na beki wao Method Mwajale kuwa majeruhi na bado hawana imani na beki Novalty Lufunga.
Simba imeshuka dimbani mara 23 na kuhhjikusanyia alama 54, huku ikikabiliwa na mchezo ugumu dhidi ya Mbeya City March 4


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt