asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Saturday, February 18, 2017

"MUGABE ANAWEZA KUPIGIWA KURA AKIWA MAITI"


Grace Mugabe na mumewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Mke wa Rais mkongwe wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amesema kuwa mumewe ni mashuhuri sana hivi kwamba anaweza kupigiwa kura hata akiwa maiti.
Bwana Mugabe, ambaye atakuwa na umri wa miaka 93 mnamo Jumanne, ametangaza mara kadhaa kuwa atagombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Grace Mugabe ana miaka 40 mchanga kwa mumewe.
Aliambia mkutano wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa hata mumewe akifariki, bado jina lake litawekwa kwenye karatasi za kupiga kura.
Alisema watu wa Zimbabwe wanampenda Rais wao sana, hivi kwamba wangempigia kura hata akiwa maiti.
Robert Mugabe
Bi Mugabe amekuwa mkosoaji mkuu wa wakosoaji wa mumewe na kwa wale walio na tamaa ya kumrithi.
Inadhaniwa kuwa alikuwa mstari wa mbele wa kumwachisha kazi aliyekuwa makamu wa rais, Joice Mujuru mwaka 2014.
Bwana Mugabe, ambeye siku hizi haonekani sana hadharani, ametawala Zimbabwe tangu taifa hilo kuwa huru miaka 37 iliyopita.

Chanzo BBC swahili


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt