asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, March 23, 2017

BAADA YA NAPE KUTUMBULIWA, GWAJIMA AJA NA MPYA...HII HAPA

Image result for gwajima
Dar esSalaam.Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.

Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema Mkuu wa Mkoa alivamia ofisi za Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.

"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.

Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt