asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Sunday, March 19, 2017

kitendawili kipya cha Hassan Kessy na Benchi la ufundi Yanga kimekuja hivi

BEKI wa pembeni wa Yanga, Hassan Kessy, amesema kipindi kile ambacho alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, alipunguza mazoezi yake binafsi kwa kile alichokuwa anaona ni kujichosha wakati akiwa hapewi nafasi.
Hivi karibuni Kessy alirejea kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina baada ya kusota kwenye benchi muda mrefu kabla ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara na nyingine mbili za kimataifa za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zanaco.
Hassan Kessy  amesema: “Nilikuwa nafanya mazoezi kujiweka sawa lakini ilifikia muda nikapunguza kufanya kutokana na kuwekwa benchi ikiwa naweza kucheza na siyo majeruhi.”
“Ninahitaji kujiongezea fiziki katika kipindi hiki ambacho tayari nina nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza ili kuisaidia timu yangu,” alisema Kessy.
Aidha mchezaji huyo wa zamani wa Simba amesema alichopanga hivi sasa kila siku atakuwa anafanya mazoezi ya binafsi ya gym na kukimbia barabarani kwa ajili ya kurejesha fiziki yake iliyopotea.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt