asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, March 13, 2017

MANCHESTER UNITED WATAUMUDU MZIKI WA CHELSEA?

Mourinho_Conte
Kocha Jose Mourinho atarejea tena darajani Stamford kesho atakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha anapata matokeo mazuri pale kikosi cha Manchester United kitakapokuwa kinacheza dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA utakaopigwa katika dimba la Stamford Bridge.
Ni kibarua kigumu kwa Mourinho, kutokana na kiwango cha Chelsea pamoja na matokeo ya mwisho baina ya mwaka jana. Oktoba mwaka jana Mourinho alikaribishwa Drajani kwa kipigo cha mabao 4-0 na Chelsea ya Antonio Conte.
Kipigo hicho kilimuudhi sana Mourinho na kumlalamikia Conte kwa kushangilia kupita kiasi.  Conte aliongoza amsha amsha za mashabiki wa Chelsea kitendo kilichomkera Mourinho kiasi cha kumvuta pembeni muitaliano huyo na kumkosoa.


Conte_01

Baada ya kipigo hicho, United waliamka na kuimarika, hawajafungwa katika mechi 17 za Ligi Kuu walizocheza tangu hapo, wamefika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Europa na pia wametwaa taji la kombe la Ligi. Kwa ujumla wamepoteza michezo miwili tu kati ya 31 waliocheza baada ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Chelsea.
Pambano dhidi ya vinara wa Ligi Chelsea ni kipimo sahihi cha ubora wa kikosi cha United licha ya wainzani wao kuwakejeli kwa kuandika kuwa ‘ Mfululizo wa matokeo ya kutopoteza katika mechi 17 mfululizo umewapandisha kutoka nafasi ya sita hadi ya sita kwenye msimamo wa Ligi’.
Huo ni utani tu wa mpira, United wameimarika baada ya Mourinho kupata chaguo la kudumu la viungo Ander Herrera na Paul Pogba.  Pia mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic amekuwa na msaada mkubwa mno katika ufungaji mabao  kufuatia kutikisa nyavu mara 26 katika mashindano yote.
Pengo la Ibrahimovic anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kwa kosa la kumpiga kiwiko Tyrone Mings ni pigo kwa United.
Ushndi dhidi ya Chelsea utakuwa ni ushahidi tosha kuwa United ni moto wa kuotea mbali kwa sasa na iko katika njia salama kurejea matawi ya juu kama ilivyokuwa enzi za Sir Alex Fergusson.
Kwa upande mwingine kipigo kitatoa picha ya umbali uliobakia kwa United kurudi kileleni na kazi kubwa anaayotakiwa kuifanya Mourinho kurudisha heshima.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt