asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Thursday, March 9, 2017

Maxime atoa tahadhari kwa Simba

Maxime akikumbatiana na mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto mara baada ya pambano lao kumalizika
KOCHA mkuu wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema  kikosi chake sasa kipo vizuri na tayari kwa ajili ya kuhakikisha kinafanya vizuri katika mechi zake zote zilizobakia katika mzungumko huu.
Maxime amesema kwamba wanataka kumaliza michuano ya ligi kuu wakiwa katika nafasi tatu za juu hivyo hawataki mchezo na tayari wakiwa wamejipanga kushinda katika mechi zao zote zilizosalia.
“Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu ya mechi za ligi kuu zilizobakia, lakini napenda kuchukua nafasi hii kusema kuwa timu zote tutakazokutana nazo katika kipindi hiki cha lala salama zinatakiwa zijipange,” alisema Maxime.
Kagera Sugar wanatarajiwa kuwaalika Simba Machi 11, kwenye Uwanja wa Kaitaba, uwanja ambao umekuwa mgumu kwa Simba kupata ushindi kwa kipindi kirefu.


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt