asali

mbogo

sawe tv

advertise

SLIDE MANENO


Usipitwe na chochote, tupo ili kukuhabarisha tembelea blog hii kila siku, pia usisahau ku subscribe youtube channel yetu ya sawe tv

Monday, March 13, 2017

Mchezaji wa zanaco aiuma sikio timu ya yanga

MTANZANIA anaeitumikia timu ya Zanaco FC ya Zambia Ayub Lyanga ambae pia ni mdogo wa mchezaji wa zamani wa Simba Daniel Lyanga amesema Yanga walicheza vizuri licha kupoteza nafasi nyingi za kufunga.
Zanako FC walilazimisha sare ya bao (1-1 ) dhidi Yanga kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa klabu bingwa Afrika.
 Ayub Lyanga amesema kwamba, wapinzania wao siyo wabaya ila walikosa umakini katika umaliziaji wa mipira pale walipopata nafasi kwenye eneo la hatari.
“Mechi ya marudiano itakuwa ngumu, ila kwa kikosi chetu kilivyo na uchu wa kufika hatua ya makundi, hivyo basi Yanga wajipange,” alisema Ayub.
Mchezaji huyo wa zamani wa Coastal Union ya Tanga alisema hakuna mchezaji aliyekuwa anasumbua kwake ila kila aliyekuwa uwanjani amecheza kwa nafasi yake


No comments:

Post a Comment

MAKTABA YA MAGAZETI / NEWSPAPER LIBRARY....... SOMA HAPA MAGAZETI YA SASA NA YALIYOPITA

  • MAGAZETI.
  • Tree in field with blue sky.
  • MAGAZETIt